Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Modi, ambaye alikuwa akihutubia taifa jana Jumamosi kwa mnasaba wa sherehe za Siku ya Uhuru wa India alisisitiza juu ya kuliimarisha jeshi la nchi hiyo na akasema, New Delhi itatoa jibu kali kwa nchi zitakazoanzisha uchokozi dhidi yake.
Waziri Mkuu wa India vilevile amesema, Pakistan ni adui wa kudumu wa nchi hiyo.
Katika hotuba yake hiyo, Narendra Modi ameihutubu pia China akisema, wanajeshi wa India wamejiweka tayari kikamilifu katika eneo la mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na China la Ladakh.
Kuhusiana na suala hilo imetangazwa kuwa, jeshi la India limetuma zana mpya za kijeshi zikiwemo helikopta kadhaa katika eneo hilo la mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na China.
Mnamo mwezi Juni mwaka huu na baada ya kushadidi mivutano kati ya China na India katika eneo hilo la mpakani ambalo hatima yake bado haijajulikana, askari 20 wa India waliuawa katika mapigano yaliyozuka baina ya pande mbili, hali ambayo ilipelekea kila upande kuongeza idadi ya wanajeshi wake katika eneo hilo la Ladakh.
Tangu mwaka 2003 hadi sasa, maafisa wa India na China wameshakutana zaidi ya mara 20 kuzungumzia tofauti zao kuhusiana na eneo hilo la mpaka wa pamoja wa nchi mbili, hata hivyo zimeshindwa kufikia makubaliano.../
342/